Je umewahi jitosa au kuelewa maana ya uchakataji wa taka? Dunia kama dunia na mazingira kwa ujumla yanakuhitaji kuyanusuru kutokana na Hali ya tabia nchi, matumizi na uhifadhi mbaya wa taka ndilo kosa kubwa ambalo linahitaji kuliangazia na kujitathmini upya kama binadamu .

Viumbe vyote vinatuhitaji kuchangia kwa kupunguza makali ya uchafuzi wa mazingira; magonjwa kama saratani ni mojawapo ya magonjwa sugu yanayoletwa kutokana na uhifadhi mbaya wa taka kwa kuchoma kemikali ambazo ni sumu .

Kuchakata taka, hasa plastiki ni njia moja inayoweza kupunguza makali ya uchafuzi wa mazingira , kwani plastiki huchukua zaidi ya miaka Mia tano kuoza, plastiki ina kemikali hatari ambazo zikichanganyika na taka zingine huchangia kwa uchafuzi wa hewa chafu na pia kuviua viumbe kwenye Mito na baharini iwapo plastiki zitapata njia ya kuingia majini.

Kwa hivyo ni jukumu letu Sote kuhakikisha tunazingatia usafi wa mazingira, kwa kununua bidhaa zilizohifadhiwa kwenye mikebe chakatishi,kupanda miti kwa wingi na pia kutambua mbebaji wako wa taka anakopeleka taka.

Hivyo tutaweza kupunguza makali ya tabia nchi kwani bila hivyo gesi zitailemea Ozoni hivyo kuleta maafa zaidi duniani kwa binadamu, wanyama na hata mimea Kwa ujumla, huu ni wakati wakujitolea kwa Nia ya kuiokoa dunia kwa Hali na Mali bila kunung’unika ,sio serikali, wananchi, mashirika yasiyo ya kiserikali Bali kila kikundi Kwa ujumla.

Tukisimama kidete kwa kushirikiana taka haitakuwa taka tena bali itakuwa ni raslimali na kuongeza ajira nyingi kuliko Hali ilivyo Kwa sasa, vijana wawe viongozi wakutajika kuichochea serikali kwa Yale manufaa ya kuwekeza kwenye Mazingira. Mazingira na Hali yenyewe ni Pana, hatuwezi kuishi bila mazingira, kila hatua ina dua kwani naona mazingira Safi usoni iwapo sote tutajitolea kuwajibika.

About Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *